×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Baba amuua mwanawe kwa kujoa kitadani huko Bondo, Siaya

Baba amuua mwanawe kwa kujoa kitadani huko Bondo, Siaya

Maafisa wa polisi wanachunguza kisa ambapo mwanamme mmoja amemuua mwanawe wa kambo mwenye umri wa miezi kumi katika eneo la Bondo, Kaunti ya Siaya kwa madai ya kukojoa kitandani.

Amemuua kisha kuutupa mwili wake chini ya kitanda.

Wakati uo huo, mvulana wa miaka kumi na minane amekamatwa kwenye Kaunti ya Nakuru kwa madai ya kumuua mwanaume wa miaka thelathini na miwili baada ya kutofautaiana kuhusu mwanamke.

Inadaiwa mshukiwa alimuua Denis Kioko kwa kumkata shingo katika mtaa wa Moi  South Lake.

Kulingana na majirani Marehemu Kioko alifika nyumbani kwa mshukiwa na kumkaripia kwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mkewe wa miaka thelathini na mitano.

Mkuu wa Polisi katika eneo hilo Samuel Waweru amesema mshukiwa aliyejeruhiwa wakati a makabiliano na marehemu anatibia katika hospitali ya Rufaa ya Naivasha na atakamatwa atakaporuhusiwa kuondoka.
Mwili umehifadhiwa katika hosptali iyo hiyo.

Kwingineko, Washukiwa wawili wa utekaji nyara wameulia katika eneo la Kabete Kaunti ya Kiambu. Wawili hao ni miongoni mwa wanne waliomteka nyara mhubiri mmoja wa kanisa la Anglikana aliyetekwa nyara jana usiku alipokuwa akielekea nyumbani.

Kulingana na polisi washukiwa waliuliwa badaa ya kukataa kutii agizo la polisi kuwataka kujisalimisha, huku wenzao wawili wakifanikia kutoroka.

Share this: