×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

EACC yawaonya wafisadi nchini

EACC yawaonya wafisadi nchini

Tume ya Maadili na Kukabili Ufisadi, EACC imewaonya maafisa wa umma ambao wanaendelea na shughuli za kikazi licha ya kukabiliwa na kesi za ufisadi na uhalifu mahakamani.

Afisa Mkuu Mtendaji wa EACC, Twalib Mbarak amewataja maafisa wanane wa Serikali ya Kaunti ya Turkana ambao wamekuwa wakienda kazini licha ya kufunguliwa kesi katika Mahakama ya Eldoret kwenye Kaunti ya Uasin Gishu. 

Maafisa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kushirikiana kuiibia Kaunti ya Turkana shilingi milioni 42.56 zilizotengwa kwa ununuzi wa gari la kukabili moto ambalo hadi sasa halijanunuliwa licha ya fedha kulipwa takriban miaka minane iliyopita.

Mbarak amesema hatua ya maafisa hao kuendelea na majukumu yao ni ukiukaji wa agizo lililotolewa na Jaji wa Mahakama Kuu, Mumbi Ngugi kwamba maafisa wanaokabiliwa na kesi wanastahili kusitisha utendakazi wao hadi kesi dhidi yao zitakaposikilizwa na kuamuliwa. 

Share this: