×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Netanyahu aapa kuendelea kuishambulia Palestine

Netanyahu aapa kuendelea kuishambulia Palestine

Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu ameapa kuendelea kutuma ndege za kivita kushambulia Palestina kwenye Ukanda wa Gaza, licha ya mashirika ya kimataifa kushauri upande wa Palestina sawa na Israeli kusitisha vita baina yao.

Mapema leo makombora ya Israeli yamewaua Wapelestina watatu katika vita hivyo ambavyo vimeingia siku ya saba.

Awali Majeshi ya Palestina yalituma roketi za kivita kuelekea Mji wa Tel Aviv nchini Israeli, na kusababisha mamia ya watu kutorokea maeneo salama.

Tayari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa UN , Antonio Guterres kwa mara nyingine ameshangazwa na mashambulizi yanayoendelea kwenye Ukanda wa Gaza kufuatia vita baina ya Israeli na Palestina.

Guterres amekashifu mashambulizi hayo ynayoendelea dhidi ya raia wasiokuwa na hatia na kusikitishwa na kushambuliwa kwa jengo moja la ghorofa kumi na tatu, ambalo lilikuwa na ofisi kadhaa za mashirika ya habari kama vile Aljaazera.

Inaarifiwa kwamba jengo hilo lilikuwa limehamwa kufuatia onyo la Israeli kwamba ingeshambulia eneo hilo.

Aidha, Guterres amesikitishwa na mauaji ya raia, vikiwamo vifo vya watu 10 wa familia moja na watoto wanane waliouliza kufuatia shambulio la usiku wa Ijumaa.

Hapo jana Rais wa Marekani Joe Biden aliwapigia simu Netanyahu wa Israeli na Rais wa Palestina Mahmoud Abbas akiwahimiza kutafuta mwafaka wa kumaliza vita baina ya mataifa hayo mawili ambayo yamekuwa yakipigana mara kwa mara.

Tangu Jumatu ilipita, Wapelestina zaidi ya mia moja na arubani na wanne wameuliwa katika eneo la Gaza, huku Waisraeli kumi wakiwamo watoto wakiuliwa kufuatia mapigano ya nchi hizo mbili.

Haya yanajiri huku hofu ikianza kutanda kuhusu uwezekano wa kuzuka kwa vita vya Intifada ya Tatu kwenye Eneo la Mashariki ya Kati, kufuatia uhasama baina ya Waisraeli na Waarabu.

Vita vya kwanza vya Intifada baina ya Palestina na Israeli vilifanyika kuanzia mwaka wa 1987 hadi 1993 kwenye Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza baina ya Waarabu na Waisraeli,  ambapo majeshi ya Israeli yaliwaua Wapelestina elfu moja, mia sita na watatu, na Wapelestina wakawaua Waisraeli mia tatu na hamsini na tisa.

Vita vya Pili vya Intifada vilifanyika kuanzia mwaka wa 2000 hadi 2005 ambapo zaidi ya Wapelstina elfu tatu waliulia na majeshi ya Israeli, huku Waisraeli takribani elfu moja wakiuliwa.

Share this: