×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Meli mbili za kwanza kutia nanga katika Bandari ya Lamu wiki hii

Meli mbili za kwanza kutia nanga katika Bandari ya Lamu wiki hii

Meli mbili za mizigo zinatarajiwa kutia nanga katika Bandari ya Lamu wiki hii. Meli hizo za Kampuni ya Maersk zitaweka historia ya kuwa meli za kwanza kuwasili nchini kupitia bandari hiyo kubwa zaidi katika Ukanda wa Afrika Mashari na Kati.

Meli ya kwanza ya Bremeharvest itatia nanga katika Bandari hiyo ikitokea Bandari ya Mombasa ikiwa na mizigo ya maparachichi huku nyingine ya MV Cap Carmel ikitia nanga ikitokea Dar Es Salaam, Tanzania ikiwa na mizigo mbalimbali.

Aidha meli ya mizigo ambayo kutia nanga kwake katika Bandari hiyo kutatumika katika shughuli ya uzinduzi tarehe ishirini mwezi huu wa mei itaondoka jijini Mombasa.

Wahandisi katika Mamlaka ya Bandari KPA wanaendelea kuweka juhudi za kufanikisha shughuli hiyo ambayo itafanyika alhamisi wiki hii.

Nahodha Mkuu wa KPA Godfrey Namadoa amesema maafisa wake watawasili kabla ya tarehe ishirini kwa ajili ya maandalizi na ukaguzi wa sehemu za kuegesha meli hizo.

Bandari ya Lamu ina sehemu ishirini na tatu za kuegesha meli za kina cha mita mia nne ndani ya maji ambapo sehemu moja imekamilika huku mbili zikitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka huu.

Share this: