×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Israel imeangusha jengo lenye ofisi za mashirika ya vyombo vya habari vya kimataifa katika Ukanda wa Gaza

Israel imeangusha jengo lenye ofisi za mashirika ya vyombo vya habari vya kimataifa katika Ukanda wa Gaza

Wanajeshi wa Israel wamedai kwamba jengo lililoangushwa kufuatia shambilio la angani katika Ukanda wa Gaza lilikuwa linatumika na wanamgambo wa Hams kuficha silaha zake za kijeshi.

Shambulio hilo lililotekelezwa saa moja baada ya Israel kutoa saa moja kwa watu kuondoka limeharibu jengo la Al-Jalaa ambako kuna ofisi za mashirika mbalimbali ya Vyombo vya Habari vya The Associated Press, Al Jazeera, AFP na vingine vya kimataifa.

Hili li shambulio la pili kutekelezwa leo hii na Israel baada ya lile la asubuhi  lililosababisha vifo vya  watu 10 wengi wao watoto.

Inasemekana kuwa hilo ndilo shambulio baya zaidi kutokea tangu kuanza kwa mapigano kati ya kundi la Hamas na Israel mapema wiki hii.

Tangu  mapigano kuanza siku ya Jumatatu, zaidi ya makombora 2,000 yamesharushwa kutokea Gaza kuelekea Israel, yakiwaua watu tisa, mmoja mtoto mdogo na mwanajeshi mmoja na kuwajeruhi watu 560.

Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ambaye anatuhumiwa  kuutumia mzozo  kujiokoa kisiasa, hadi sasa hajaoneshara ishara yoyote ya kulegeza  mashambulio ya kijeshi dhidi ya Gaza.

Hadi sasa, Israel inasema imeshapiga maeneo takribani 800 ndani ya Ukanda wa Gaza, ikiwamo njia ya chini inayotumiwa na wanamgambo wa Hamas.

Kufikia asubuhi ya  leo Israel ilikuwa inakisia kuwa ilishafanikiwa kuwaua zaidi ya makamanda 30 wa Kipalestina .

Tayari mazungumzo ya kutafuta mwafaka ya mzozo huo yameanza leo huku Marekani ikishauriana na wawakilishi wa Israel, Palestina na maafisa wa Umoja wa mataifa .

Hapo jana Baraza la Usalama lamoja wa Mataifa litafanya kikao kingine cha kutafuta mwafaka.

Kulingana na Umoja wa mataifa  zaidi ya wakazi 10,000 wa Gaza wamelazimika kuhama makazi yao wakihofia usalama.

Share this: