×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais Kenyatta yuko Ethiopia kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Guelleh

Rais Kenyatta yuko Ethiopia kuhudhuria kuapishwa kwa Rais Guelleh

Rais Uhuru Kenyatta yuko nchini Djibouti kuhudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais Ismail Omar Guelleh.

Rais Kenyatta ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Muungano wa Afrika Mashariki ameandamana na Waziri wa Mashauri ya Nchi za Kigeni Raychelle Omamo.

Ni wiki ii hii tu ambapo Rais amehudhuria hafla ya kuapishwa kwa Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Viongozi wengine ambao wako Djibouti kwa hafla hiyo ni Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, Rais wa Somaliland Muse Biihi, Waziri Mkuu wa Somalia Mohamed Roble miongoni mwa wengine.

Aidha, waziri mkuu wa Rwanda Édouard Ngirente, anatarajiwa kuwasili kumwakilisha Rais Paul Kagame .

Rais Guelleh alishinda katika uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi April ambapo alipata zaidi ya asilimia 98 ya kura zote zilizopigwa na kumshinda aliyekuwa mpinzani wake wa karibu Zakaria Ismail Farah .

Guelleh amekuwa Rais wa Djibouti tangu mwaka wa 1999.

Share this: