×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Nairobi, Alex ole Magelo anazikwa Jumamosi

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Nairobi, Alex ole Magelo anazikwa Jumamosi

Aliyekuwa Spika wa Bunge la Nairobi Alex Ole Magelo   na Mwenyekiti wa Klabu ya Soka ya AFC Leopards anazikwa nyumbani kwake Jumamosi .

Ole Magelo ambaye aliaga dunia akiwa na miaka sitini na saba, atazikwa katika Kijiji cha Kipeto kwenye kaunti ya Kajiado.

Viongozi mbalimbali wa kisiasa wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo akiwamo Gavana wa Kajiado Joseph Ole Lenku.

Marehemu Ole Magelo aliaga dunia Jumamosi iliyopita alipokuwa akitibiwa katika Nairobi Hospital baada ya kuugua kwa muda mfupi.

Magelo aliwahi kuwa Diwani Jijini Nairobi, kisha kuwa Mwenyekiti wa AFC Leopards, kabla ya kuteuliwa kuwa spika wa Bunge la Nairobi kuanzia mwaka wa 2013 hadi 2017.

Share this: