×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Baraza la Umoja wa Mataifa linafanya kikao kufuatia mapigano baina ya Israel na Palestine

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa leo hii linatarajiwa kufanya kikao cha dharura ili kuangazia hali ilivyo katika eneo la Mashariki ya Kati kwa lengo la kusulushisha mzozo unaoendelea baina ya taifa la Israeli na Palestina katika Ukanda wa Gaza,  ambao umesababisha vifo vya watu zaidi ya mia moja huku wengine wakijeruhiwa

Kikao cha leo kinajiri wakati ambapo Israeli inaendelea kushambulia Ukanda wa Gaza kwa kutuma ndege zaidi ya mia moja sitini za kivita, huku wanamgambo wa Hamas kutoka Palestina wakiendelea kurusha makombora kuelekea Israeli.

Mkutano huo unatarajiwa kuwa wa wazi na ambao utawashirikisha wawakilishi wa Israeli na Palestina, ingawa hadi sasa Marekani haijatoa hakikisho la kuhudhuria.

Tayari Baraza hilo limeitisha vikao viwili kwa njia ya video tangu Jumatatu, ambapo cha leo kitakuwa cha tatu huku Marekani ikipinga kutolewa kwa tamko la pamoja ambalo huenda likachochea hali kuwa mbaya hata zaidi.

Hata hivyo, inaarifiwa kwamba Israeli ambayo inaungwa mkono na Marekani, imepinga Baraza hilo kujihusisha na mgogoro huo kwa lengo la kusitisha mapigano.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la DW, Jeshi la Israeli limewaua Wapalestina sita katika saa ishirini na nne zilizopita, akiwamo mmoja ambaye amedaiwa kujaribu kumdunga kisu mwanajeshi wa Israeli.

Kufikia sasa, zaidi ya watu mia moja na kumi na tisa wameuliwa na Wanajeshi wa Israeli, huku Wapelestina wakiwaua Waisraeli wanane pekee tangu mapigano hayo yalipoanza Jumatatu.

Share this: