×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mudavadi awataka wataalamu kuchambua uamuzi wa kusitisha mpango wa BBI

Mudavadi awataka wataalamu kuchambua uamuzi wa kusitisha mpango wa BBI

Kinara wa ANC Musalia Mudavadi amesema kwamba pana haja ya wataalam wa masuala ya kisheria na mawakili kuchanganua kwa undani uamuzi wa kusitisha mchakato wa BBI.

Akizungumza katika eneo Bunge la Kilgoris kwenye Kaunti ya Narok, wakati wa kikao na wazee na viongozi wa Jamii ya Maasai , Mudavadi amesema licha ya mahakama kusema kwamba mchakato wa BBI haukuzingatia sheria pana haja ya matakwa ya umma kufanywa kipau mbele.

Mudavadi vilevile amesema kwamba baadhi ya masuala katika BBI yameonekana kuingizwa siasa.

Hata hivyo, amewasuta vikali wanaoneza propaganda kwamba Rais Uhuru Kenyatta amepoteza uungwaji mkono wa Wakenya baada ya kuwatelekeza.

Kiongozi huyo amesema kwamba ni muhimu kwa sasa kwa Wakenya kuendelea kuungana na kushirikiana kwa manufaa ya maendeleo ya nchi. Amewashauri Wakenya kutuliza joto la kisiasa na kuishi kwa amani kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Mudavadi aliyekutana na wazee hao nyumbani kwake aliyekuwa Waziri na mbunge Julius Sunkuli, vile vile alitumia fursa hiyo kuwaomba wenyeji wa Kilgoris, na jamii ya Maasai kuunga azma yake mkono ya kuwania urais mwaka ujao.

Ameahidi kuangazia malalamiko yao wakati atatwaa uongozi wa taifa.

Share this: