×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kamati ya BBI kukata rufaa kuhusu uamuzi wa kusitisha mpango huo

Kamati ya BBI kukata rufaa kuhusu uamuzi wa kusitisha mpango huo

Kamati ya Kitaifa inayoendesha mpango wa kuifanyia katiba marekebisho kupitia BBI imepinga uamuzi wa Mahakama Kuu ambao uliharamisha mchakato huo huku ikipanga kuwasilisha rufaa mahakamani wiki ijayo.

Katika taarifa, wenyekiti wa kamati hiyo ya BBI, Junet Mohammed na Dennis Waweru wamesema wanaheshimu uamuzi uliotolewa na jopo la majaji watano kuharamisha mchakato huo japo hawakubaliani nao.

Junet amewasuta majaji hao kwa kusema kwamba Rais anaweza kushtakiwa kwa kushinikiza marekebisho ya katiba kupitia BBI.

Amewasihi wananchi kusalia watulivu akisema katiba itafanyiwa marekebisho kupitia BBI kwani ndio mustakabali wa taifa.

Tayari Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Paul Kihara Kariuki na Wakili Ken Ogeto wamesema watakata rufaa kupinga uamuzi huo wa mahakama ili kuendeleza mipango ya kura ya maamuzi.

Kisheria uamuzi wa Mahakama Kuu unaweza kubatilishwa katika Mahakama ya Rufaa na iwapo utadumishwa bado mlalamishi anaweza kuwasilisha rufaa hiyo katika Mahakama ya Juu.

Ikumbukwe majaji Joel Ngugi, George Odunga, Jairus Ngaaah, Chacha Mwita na Teresia Matheka walisema Rais Kenyatta alikiuka katiba na kwamba anaweza kushtakiwa hata akiwa madarakani.

Share this: