×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu 392 waambukizwa korona huku 8 wafariki dunia

Watu 392 waambukizwa korona huku 8 wafariki dunia

Kiwango cha maambukizi ya virusi vya korona nchini kimesalia asilimia kumi kwa siku pili sasa.

Katika kipindi cha saa ishirini na nne zilizopita, watu 392 wamethibitishwa kuambukizwa virusi hivyo kufuatia vipimo vya sampuli 3, 668.

Watu 383 miongoni mwao ni Wakenya huku 9 wakiwa raia wa mataifa mengine.

Aidha mdogo zaidi miongoni mwa walioambukizwa ni mtoto mwenye umri wa miezi miwili huku mkongwe akiwa na miaka 95.

Jumla ya waliombukizwa imefikia watu 165, 112.

Kupitia taarifa, Wizara ya Afya imesema watu 184 wamepona Covid-19, 152 walikuwa wakihudumiwa nyumbani na 32 kwenye hospitali mbalimbali.

Hata hivyo, watu wengine 8 wamefariki dunia, mmoja katika saa ishirini na nne zilizopita na 7 kwenye hospitali mbalimbali nchini katika siku tofauti toafuti.

Idadi hii sasa inafikisha jumla ya waliofariki dunia kutokana na COVID-19 kuwa watu 2,976.

Kufikia sasa jumla ya watu 1,040 wamelazwa kwenye hospitali mbalimbali, 118 wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi, 23 wamewekewa vipumuzi, 74 hewa ya oksijeni na 21 wanahitaji uangalizi wa karibu.

Kuhusu chanjo, watu 933,436 wamechanjwa kufikia leo.

Wizara imesema miongoni mwao 287,411 ni wakongwe, 162,396 wahudumu wa afya, 146,538 ni walimu, 78,906 maafisa wa polisi na 261, 185 ni Wakenya wengine.

Share this: