×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Miili ya watu wawili miongoni mwa wanne waliokufa maji mtaani Kibra imeopolewa

Miili ya watu wawili miongoni mwa wanne waliokufa maji mtaani Kibra imeopolewa

 Mili ya watu wawili ambao ni miongoni mwa wanne waliosombwa na mafuriko katika mtaa wa Kibra jijini Nairobi imepatikana katika eneo la Silanga kwenye mtaa huo.

Kamanda wa Polisi wa Nairobi, Augustine Nthumbi amesema juhudi za kuitafuta mili ya watu wengine zinaendelea huku ikihofiwa kwamba huenda kuna watu zaidi waliosombwa.

Aidha, watu wengine wawili walisombwa na mafuriko katika Mtaa wa Mukuru Kayaba kwenye Eneo Bunge la Starehe.

Mbunge wa eneo hilo, Charles Njagua amesema juhudi za kuwasaidia waathiriwa wa mafuriko hasa wanaoishi karibu na maeneo ya mto zinaendelea.

Baadhi ya wakazi wanaoishi karibu na mto huo hata hivyo wamesema hawajui pakwenda kutafuta hifadhi kipindi hiki cha mvua.

Mvua iliyonyesha ilichangia kupotea kwa nguvu za umeme katika maeneo takriban kumi jijini Nairobi yakiwamo Nairobi West, South C, Barabara ya Lang'ata na ile ya Mbagathi baada ya kituo cha usambazaji umeme kilichoko katika eneo la Nairobi West kufurika maji.

Mhandisi katika Kampuni ya Kenya Power Charles Mwaura amesema juhudi zimekuwa zikiendelea za kurejesha umeme katika maeneo ambayo yameathirika.

Idara ya Utabiri wa Hali ya Anga imesema mvua kubwa ambayo imekuwa ikishuhudiwa inatarajiwa kupungua kati ya leo na kesho japo kuonya kuhusu mafuriko na maporomoko ya ardhi.

Katika Kaunti ya Kirinyaga, Mkurugenzi wa Utabiri wa Anga, Peter Wambugu amewashauri wanaoishi katika nyanda za chini kuhamia maeneo ya juu kwani huenda maporomoko ya ardhi yakashuhudiwa. 

Share this: