×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kenyatta amemteua rasmi Jaji William Ouko kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu

Kenyatta amemteua rasmi Jaji William Ouko kuwa Jaji wa Mahakama ya Juu

Rais Uhuru Kenyatta amemteua rasmi Rais wa Mahakama ya Rufaa, William Ouko kuwa Jaji katika Mahakama ya Juu.

Uteuzi wake umejiri baada ya Tume ya Huduma za Mahakama, JSC kumwidhinisha kwa wadhifa huo baada ya kuwafanyia mchujo watu tisa.

Ouko atachukua nafasi ya Jaji Jackton Ojwang' ambaye alistaafu mwezi Februari mwaka uliopita akia na mika sabini. 

Jaji Ouko aliteuliwa kuhudumu katika Mahakama ya Rufaa mwaka 2012 kabla ya kufanywa rais wa mahakama hiyo Machi 9 mwaka 2018.

Hayo yanajiri huku Jaji Mkuu Mteule, Martha Koome akisubiri uamuzi wa Kamati ya Haki na Sheria, JLAC katika Bunge la Kitaifa wa iwapo ataidhinshwa ama la.

Kamati hiyo ilimfanyia mchujo hapo jana baada ya jina lake kuwasilishwa bungeni na Rais aliyepokea pendekezo la uteuzi wake kutoka kwa JSC.

Share this: