×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Vikao vya kusikiliza na kutathmini hoja ya kumbandua Gavana wa Wajir Mohammed Abdi vinaanza Jumatano

Vikao vya kusikiliza na kutathmini hoja ya kumbandua Gavana wa Wajir Mohammed Abdi vinaanza Jumatano

Vikao vya kusikiliza na kutathmini hoja ya kumbandua Gavana wa Wajir Mohammed Abdi vinaanza leo Jumatano.

Seneta wa Nyamira Okong'o Omogeni ataongoza kamati ya watu 11 kusikiliza hoja hiyo kabla ya kuwasilisha majibu katika Seneti.

Wanachama wengine ni; Susan Kihika ambaye ni Naibu Mwenyekiti, Johnson Sakaja, Mwangi Githiomi, Christine Zawadi, Mithika Linturi, Hargura Godana, Fred Outa, Agnes Muthama, Petronilla Were na Issa Juma Boy.

Tayari Bunge la Wajir limewateua wawakilishi watatu katika kesi hiyo amba ni Andullahi Isaack, Shub Barre Ahmed na Hussein Abdirahman Dahi.

Ushahidi zadi unatarajiwa kutoka kwa Khaire Omar Maalim, Yussuf Mohamed Abdi Barhiya Mohamed Abd na Osman Abdi Jinale. Wakili Ahmednassir Abdullahi anatarajiwa kuongoza jopo la mawakili katika kesi hiyo.

 

Miongoni mwa tuhuma zinazomwandama Gavana Abdi ni matumizi mabaya ya mamlaka, mapendeleo ya kifamilia katika utoaji zabuni na katika maamuzi yake miongoni mwa mengine.

Share this: