×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mswada wa BBI kuwasilishwa kwa Rais baada ya kupitishwa bungeni

Mswada wa BBI kuwasilishwa kwa Rais baada ya kupitishwa bungeni

Mswada wa marekebisho ya katiba wa mwaka 2020 sasa unatarajiwa kuwasilishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta ili kutiwa saini baada ya kupita katika mabunge ya Seneti na Kitaifa.

Bunge la Seneti lilipitisha mswada huo hapo jana kwa kura 52 dhidi ya 12 za waliopinga  ikiwa ni siku chache baada ya Bunge la Kitaifa kufanya vivyo hivyo. Kisheria, Rais anaweza kuchapisha mswada huo kuwa sheria chini ya kipindi cha siku 30 iwapo haigusi vipengele vya sehemu ya 255 vinavyolazimu Kura ya Maamuzi.

Hata hivyo, iwao inagusia vipengele hivyo, ataiomba Tume ya Uchaguzi, IEBC kuadaa Kura ya Maamuzi chini a kipindi cha siku 90 kisha kutia saini baada ya Kura ya Maamuzi iwapo mswada huo utakuwa umepita.

Hata hivyo kizingiti kikuu katika kufanyika Kura ya Maamuzi ni kesi zilizowasilishwa  kupinga mchakato huo na ambazo zinaamuliwa hapo kesho.

Mwezi Februari, majaji Joel Ngugi, George Odunga, Jairus Ngaah, Janet Mulwa na Chacha Mwita waliagiza kwamba shughuli ya kujadili mswada huo katika mabunge ya Kitaifa na Seneti inaweza kuendelea japo walizuia Tume ya Uchaguzi, IEBC kuandaa Kura ya Maamuzi hadi kesi hiyo isikilizwe na kuamuliwa.

Kesi hizo ndizo zilikuwa kizingiti kikuu katika mchakaato mzima wa mswada wa BBI baada ya kupitishwa katika Bunge la Kitaifa na unatarajiwa pia kupitishwa katika Seneti. Baadhi ya kesi hizo zinakosoa jinsi mswada huo ulivyoasisiwa.

Share this: