×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Havi akosolewa kwa madai ya kutumia LSK kwa manufaa ya kisiasa

Havi akosolewa kwa madai ya kutumia LSK kwa manufaa ya kisiasa

Mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yameendelea kumkosoa Rais wa Chama cha Wanasheria, LSK Nelson Havi ambaye anapinga uteuzi wa Jaji Martha Koome kuwa Jaji Mkuu.

Mkurugenzi wa Shirika la Center for Human Rights and Democracy CHRD Kipkorir Ng'etich anasema Havi hafai kuingiza siasa katika mchakato wa Tume ya Huduma za Mahakama JSC kumtafuta jaji mkuu baada ya David Maraga kustaafu.

Ng'etich ameeleza haja ya Havi kutumia mbinu bora za kushauri taasisi za umma badala ya kuibua uhasama baina ya LSK na serikali.

Ni juzi tu ambapo Jaji Koome alitishia kumshtaki Havi akisema amemdhalilisha baada ya kusema kwamba hawezi kujifanyia maamuzi bila shinikizo la watu fulani serikalini.

Alipopinga uteuzi wa Jaji Koome, Havi alisema JSC ilikosa kufuata sheria katika kumteua Jaji Mkuu miongoni mwa waliowasilisha maombi.

LSK ilitaka JSC kuweka wazi kwa umma alama za wote waliohojiwa huku Wakili Maarufu Fred Ngatia akidai kwamba makamishna wa JSC walibadili alama zake alizopata wakati wa mahojiano ili kumwangusha na kumpendelea Koome.

Ikumbukwe wananchi wana hadi tarehe 12 Mei kuwasilisha malalamishi yoyote kuhusu Jaji Mkuu Mteule, Martha Koome kabla ya kufanyiwa mchujo na Bunge la Kitaifa tarehe 13 Mei

Share this: