×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kenya yapokea Suluhu kwa mara ya kwanza akiwa rais

Kenya yapokea Suluhu kwa mara ya kwanza akiwa rais

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameanza rasmi ziara ya siku mbili za kikazi nchini Kenya kwa mara ya kwanza, baada ya kupokelewa na Rais Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi.

Mizinga 21 imepigwa na wanajeshi wa Kenya kwa heshima ya Rais Suluhu ambaye ni mwanamke wa kwanza kuwa Rais katika Jumuia ya Afrika Mashariki, kufuatia kifo cha Hayati John Pombe Magufuli.

Aidha, Suluhu amekagua gwaride la heshima lililofanywa na Majeshi ya Ulinzi, KDF akiwa Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania.

Marais Kenyatta na Suluhu wanatarajiwa kutoa taarifa ya pamoja muda wowote kuanzia sasa baada ya kufanya kikao cha faragha katika juhudi za kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.

Tofauti na ilivyotarajiwa, msafara wa Suluhu haukutumia Barabara Kuu ya Mombasa baada ya Rais huyo kuwasili nchini humu majira ya saa nne asubuhi.

Alipotua katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Jomo Kenyatta JKIA  kwa Ndege ya Tanzania Air, Suluhu ambaye amepokelewa na Mawaziri Raychelle Omamo wa Masuala ya Nchi za Kigeni na Amina Mohammed wa Michezo, alitumia Barabara za Southern Bypass, Lang'ata kisha Mbagathi Way kabla ya kuingia katika Ikulu ya Nairobi.

Inaarifiwa kwamba Rais huyo alitumia barabara mbadala ya takribani kilometa kumi, ili kukwepa Barabara ya Mombasa ambayo bado inajengwa kufuatia Ujenzi wa Nairobi Expressway, ambapo kwa kigezo cha usalama kiongozi wa nchi hafai kutumia barabara inayofanyiwa ujenzi.

Msafara wa Suluhu umesababisha msongamano mkubwa wa magari kenye Barabara Kuu ya Mombasa, hali ambayo imewalazimu madereva kutumia babara mbadala za Industrial Area, Jogoo Road na South B ili kuingia na kutoka jijini.

Miongoni mwa shughuli ambazo Suluhu anatarajiwa kushiriki ni Kongamano la Kina Mama Wafanyabiashara na mijadala ya kuangazia uhusiano wa kidiplomasia na mwenyeji wake Kenyatta.

Jumane jioni, Rais Kenyatta na Mkewe Bi. Margret Kenyatta watashiriki mlo wa pamoja na Rais Suluhu katika Ikulu ya Nairobi.

Jumatano, Suluhu anatarajiwa kuhutubia kikao cha pamoja cha wabunge na maseneta, na tayari maspika Justin Muturi wa Bunge la Kitaifa na mwenzake Ken Lusaka wa Seneti wamechapisha katika gazeri rasmi la serikali kikao hicho kitakachong'oa nanga saa nanu unusu katika majengo ya bunge.

Share this: