×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Jaji Nderi ahojiwa na JSC kujaza nafasi ya Mahakama ya Juu

Jaji Nderi ahojiwa na JSC kujaza nafasi ya Mahakama ya Juu

Mahojiano ya kumsaka Jaji wa Mahakama ya Juu yaliingia siku ya pili Jumanne ikiwa ni zamu ya Jaji wa Mahakama ya Uajiri na Leba, Nduma Nderi na Dkt. Partrick Lumumba.

Jaji Nderi ametakiwa kufafanua uelewa wake kuhusu majukumu yanayostahili kutekelezwa na Mahakama ya Juu ambapo amesema miongoni mwa majukumu hayo ni kuhakikisha kesi mbalimbali hasa za uchaguzi zinashughulikiwa kwa wakati ili kuepusha mgogoro wa kiuchumi.

Jaji Nderi aidha ametakiwa kutoa msimamo wake kuhusu masuala kadhaa. Miongoni mwa masuala hayo ni jukumu linalostahili kutekelezwa na wazazi katika malezi ya mtoto hasa endapo wazazi hao hawajaoana.

Nderi amesema kila mzazi ana jukumu kuu badala ya kumwachia mzazi mmoja majukumu yote. Swali hilo limeulizwa na Kamishna wa Tume ya Huduma za Mahakama, JSC Everlyne Olwade.

Jaji Nderi amesema anayaelewa fika majukumu yake huku akisisitiza umuhimu wa Mahakama ya Juu kuwa na majaji kutoka vitengo mbalimbali vya Idara ya Mahakama akisema hilo litafanikisha utoaji wa maamuzi mwafaka kuhusu kesi zinazowasilishwa katika Mahakama ya Juu.

Kwa upande wake, Dkt. Partick Lumumba amesema anatambua fika tatizo kuu katika Idara ya Mahakama ambalo amelitaja kuwa utaratibu unaotumiwa katika kesi. Amesema utaratibu huo umekuwa na miingilio hali inayochangia ufisadi na kwamba iwapo atakuwa Jaji katika Mahakama ya Juu, ana suluhu la kuyalainisha mambo katika mahakama kwa kipindi cha miezi sita

Wengine waliohojiwa jana ni majaji Said Chitembwe na Marete Njagi. 

Share this: