×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Migawanyiko yaendelea kuzuka ODM kuhusu BBI

Migawanyiko yaendelea kuzuka ODM kuhusu BBI

Msimamo wa Seneta wa Siaya James Orengo kuhusu Mswada wa Marekebisho ya Katiba wa mwaka 2020 unaendelea kuzua mgawanyiko katika ODM ambapo amedaiwa kuwa msaliti.

Seneta huyo ambaye vilevile ni Kiongozi wa Wachache katika Seneti amekuwa mstari wa mbele kusisitiza haja ya BBI kufanyiwa mabadiliko ili kuwanufaisha wakazi wa baadhi ya maeneo likiwamo Nyanza ambayo anahisi ilivyo sasa hayatanufaika.

Akizungumza katika Kaunti ya Siaya, Orengo alidokeza kwamba anashinikiza kutumika kwa takwimu za Taasisi ya Kitaifa ya Takwimu KNBS ambazo zinatoa taswira yenye usawa zaidi katika ugavi wa maeneo bunge mapya. 

Orengo alikuwa ametetea hayo katika mjadala wa seneti sawa na mbunge wa Rarieda Otiende Amollo, Tom Kajwang wa Ruaraka, Millie Odhiambo wa Suba Kusini miongoni mwa wengine.

Hata hivyo, kauli yake imepingwa na Mwenyekiti wa ODM John Mbadi na Kiongozi wa Uchaguzi vilevile Mbunge wa Ugunja Opiyo Wandayi wakisisitiza msimamo wa chama ni mswada wa BBI kupitishwa jinsi ulivyo na maeneo bunge mapya 70 kuwa vilevile pasi na mabadiliko.

Licha ya mivutano hiyo, awali Orengo alinukuliwa waziwazi akipigia debe mswada huo kupitishwa jinsi ulivyo hali iliyoleta mkanganyiko hata zaidi.

Share this: