×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais Suluhu awasili Kenya kwa ziara ya kwanza

Rais Suluhu awasili Kenya kwa ziara ya kwanza

Rais wa Tanzania Samia Suluhu aliwasili Kenya siku ya Jumanne katika ziara ya siku mbili ambayo ni ya kwanza akiwa rais.

Siku inayofuata, Suluhu  atahutubia kikao cha pamoja cha wabunge na maseneta, na tayari maspika Justin Muturi wa Bunge la Kitaifa na mwenzake Ken Lusaka wa Seneti wamechapisha katika gazeri rasmi la serikali kikao hicho kitakachong'oa nanga saa nane unusu.

Aidha, kwa upande wake, Lusaka alisitisha kikao kilichoratibiwa na Seneti kujadili Mswada wa Marekebisho ya Katiba Mwaka 2020 na badala yake kujadili Mswada wa Ugavi wa mapato kwenye Kaunti, ili kutoa fursa kwa Suluhu kuhutubu.

Baada ya kuwasili, Suluhu atakukutana na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta ambapo masuala mbalimbali yanatarajiwa kujadiliwa ikiwemo biashara na uhusiano wa kidiplomasia kati ya Kenya na Tanzania.

Share this: