×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Usaili wa kumsaka jaji wa Mahakama ya Juu wang'oa nanga

Usaili wa kumsaka jaji wa Mahakama ya Juu wang'oa nanga

Shughuli ya kumsaka Jaji wa Mahakama ya Juu atakayeijaza nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Jacton Ojwang aliyestaafu imeanza leo ambapo Majaji Said Chitembwe na Marete Njagi wamehojiwa.

Katika vikao vya leo ambavyo vimechukua takribani saa nne kwa kila mwanianji, Jaji Said Chitembwe amekuwa wa kwanza kufika mbele Kamati ya Makamishna wa Tume ya JSC. Kamishna Mohamed Warsame amemtaka Chitembwe kutoa mfano wa kesi ambazo ziliamuliwa na Mahakama ya Juu ambazo maamuzi yake anahisi kwamba hayakuzingatia sheria.

Chitembwe akisema kuwa kufikia sasa hajui sababu zilizowafanya majaji sita wa mahakama hiyo walioafikia uamuzi wa kuufuta uchaguzi wa Urais mwaka 2017. Kwa mujibu wa Chitembwe uamuzi wa Jaji Njoki Ndung'u wa kupinga kufutwa kwa ushindi wa Rais ndio ulioweka wazi hoja za kuutetea.

Aidha Chitembwe ametakiwa kufafanua jinsi alivyoafikia uamuzi wa kuwataka wasanii kujichagulia mfumo wa kuwasilishwa kwa malipo yao punde kazi zao zinapotumiwa na kampuni mbalimbali. Kesi hiyo inayohusu sheria za hakimiliki Copyright laws ilihusisha kampuni moja ya mwasiliano nchini mwaka 2016.

Kwa upande wake Jaji Marete Njagi ametakiwa kueleza suala la ni nani mwenye haki ya kumlea mtoto ambaye amezaliwa katika ndoa ambayo, baba alikubali mkewe kupata uja uzito na mwanamume mwingine kutokana na sababu mbalimbali yaani Surrogacy.

Swali hilo ambalo limeulizwa na Kamishna Everlyn Olwande, limemfanya Jaji Marete kukiri kuwa gumu kulijibu. Imemlazimu Kamishna Olwande kumtaka Marete kuweka wazi haki za mwanamke aliye katika ndoa na yule waliyeafikiana na mumewe kumzaa mtoto.

Aidha, suala la muda ambapo Mahakama ya Rufaa na Mahakama ya Juu zinaweza kushughulikia kesi kwa wakati mmoja pia limeibuliwa katika mahojiano hayo.

Wakati uo huo,  Marete ametakiwa kuweka wazi jinsi atakavyoshughulikia madai ya ukabila endapo atatueuliwa kuwa Jaji wa mahakama hiyo, ikizingatiwa kuwa wiki jana JSC ilimteua Jaji Martha Koome kutoka Eneo la Mlima Kenya kuwa Jaji Mkuu.

Mahojiano hayo yataendelea kesho kwa Jaji Nduma Nderi kuhojiwa kuanzia saa tatu hadi saa nne asubuhi kabla ya Nyaberi Justry Patrick Lumumba kuanzia saa tano asubuhi hadi saa nane mchana. Wengine watakaohijiwa ni majaji William Ouko, Joseph Kiplagat na Yano Alice Jepkoech.

Ikumbukwe Majaji, Chitembwe, Nduma Nderi na Yeno Alice walikuwa katika mahojiano ya kumtafuta Jaji Mkuu, wadhifa ambao ulikabidhiwa Jaji Martha Koome anayesubiri Bunge kumwidhinisha kabla ya Rais Kenyatta kumwapisha.

Share this: