×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Omtata aitaka mahakama kumzuia Karani wa Bunge kuendelea kuhudumu

Omtata aitaka mahakama kumzuia Karani wa Bunge kuendelea kuhudumu

Mahakama imetaja kuwa ya dharura kesi ya kupinga hatua ya Kamati ya Huduma za Bunge la Kitaifa, PSC kumwongezea kandarasi Karani wa Bunge, Michael Sialai.

Kesi hiyo imewasilishwa na Mwanaharakati, Okiya Omtatah ambaye anasema Sialai anapaswa kustaafu wala si kuendelea kuhudumu katika nafasi hiyo.

Amesema PSC imekiuka sheria hivyo mahakama inapaswa kuishurutisha kusitisha mpango huo.

Wiki iliyopita, kamati hiyo ilimwongezea Sialai kandarasi ya kuhudumu. Hii ina maana kwamba kandarasi hiyo mpya itaanza Februari mwaka ujao.

Katika taarifa iliyotumwa bungeni, Katibu wa PSC Jeremiah Nyegenye alitangaza kuteuliwa tena kwa Sialai.

Nyegenye alisema kuteuliwa tena kwa Sialai ni kuruhusu shughuli za bunge kuendelea bila matatizo yoyote.

Share this: