×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Watu wengine 137 waambukizwa virusi vya korona

Watu wengine 137 waambukizwa virusi vya korona

Kwa siku ya pili, kiwango cha maambukizi ya virusi vya korona kimesalia kuwa asilimia 8.3 baada ya watu wengine mia moja thelathini na saba kuambukizwa kutokana vipimo vya sampuli elfu moja, mia sita arubaini na moja. Kiwango hiki kimeshuka kwa asilimia 4.5 ya Jumamosi. Idadi ya leo inawajumuisha Wakenya mia moja ishirini na tisa na raia wanane wa kigeni.

Kwa jumla watu walioambukizwa korona nchini wamefikia elfu mia moja sitini, mia tano hamsini na tisa. Katika takwimu za leo, Wizara ya Afya aidha imesema wagonjwa elfu moja, mia mbili sitini na watano wamelazwa hospitalini, elfu sita mia sita kumi na wanne wanaendelea kuhudumiwa nyumbani. Aidha, wagonjwa mia moja sabini na tisa wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi ambapo wanane wanahitaji uangalizi wa karibu.

Aidha wagonjwa wengine mia mbili kumi na sita wa Covid-19 wamepona, ambapo mia moja na sabini walikuwa wakihudumiwa nyumbani na arubaini na sita kwenye hospitali mbalimbali. Kwa jumla waliopona sasa ni elfu mia moja na tisa na sabini na saba.

Wakati uo huo, wagonjwa wengine kumi na wanane wameripotiwa kufariki dunia kutokana na makali ya Covid-19. Tisa walifariki katika siku tofauti tofauti mwezi huu, na wengine tisa wakiwa wale waliothibitishwa baada ya kufanyiwa vipimo walipofariki kwenye hospitali mbalimbali. Kwa jumla waliofariki dunia ni elfu mbili, mia saba themanini na mmoja.

Haya yanajiri huku Wizara ya Afya ikisema watu elfu mia nane themanini na saba na thelathini na wanne wamechanjwa dhidi ya korona kufikia sasa. Watu wenye umri wa miaka 58 waliochanjwa ni elfu mia tano kumi na sita, mia sita kumi na sita, wahudumu wa afya wakiwa elfu mia moja hamsini na nane, mia moja sitini na wanane.

Aidha walimu ni elfu mia moja thelathini na saba, mia saba na mmoja huku maafisa wa usalama wakiwa elfu sabini na nne, mia tano hamsini na wanne.

Share this: