×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mashirika ya habari yashauriwa kuboresha mazingira ya wanahabari

Mashirika ya habari yashauriwa kuboresha mazingira ya wanahabari

Spika wa Bunge la Kitaifa, Justine Muturi ameushauri uongozi wa mashirika ya habari nchini kuhakikisha kuwa pana mazingira mazuri ya kufanyia kazi kwa wanahabari.

Akizungumza wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari, Spika Muturi amesema pana haja ya mashirika hayo  kuwalipa vyema wanahabari ili kuwapa motisha ya kuendeleza shughuli zao.

Muturi amesema mengi yamekuwa yakiwakandamiza wanahabari na kwamba wakati umefika wa kuwalipa vyema.

Nalo Baraza la Vyombo vya Habari nchini, limetoa changamoto wa Wanahabari kutekeleza wajibu wao ifaavyo kwa kuzingatia sheria za uanahabari.

Shirika hilo vilevile,  limelalamikia kupuuzwa kwa uhuru wa vyombo vya habari na kukandamizwa kwa haki zao na hata wanahabari wengine kudhulumiwa wakati wa kutekeleza wajibu wao

Licha ya kuwapo kwa dhuluma kadhaa na ukandamizaji wa haki za vyombo vya habari, uhuru wa vyombo vya habari humu nchini hauwezi kulinganishwa na mataifa kama vile Ghana, Afrika Kusini na Naigeria.

Siku hii ilianza kuadhimishwa mwaka wa 1993 kuangazia changamoto na mikakati iliyopigwa na mataifa kulinda uhuru wa vyombo vya habari

Share this: