×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Chitembwe aukosoa uamuzi wa kuufutiliwa mbali uchaguzi wa urais wa 2017

Chitembwe aukosoa uamuzi wa kuufutiliwa mbali uchaguzi wa urais wa 2017

Jaji wa Mahakama Kuu Said Chitembwe ameukosoa uamuzi wa Mahakama ya Juu wa kuufutilia mbali uchaguzi wa Urais wa mwaka 2017 akisema kufikia sasa hajazielewa sababu zilizosababisha kuafikiwa kwa uamuzi huo.

Chitembwe ambaye ni miongoni mwa majaji ambao waliohojiwa kwa wadhifa wa Jaji Mkuu vilevile ule wa Jaji katika Mahakama ya Juu ameweka wazi kwamba aliridhishwa na uamuzi na hoja zilizotolewa na Jaji Njoki Ndung'u ambaye aliamua kwamba uchaguzi huo ulifanyika kwa kuzingatia sheria.

Aidha ameshangazwa na hatua ya Mahakama ya Juu kukosa kusuluhisha kesi inayohusu stakabadhi za kielimu za Gavana wa Wajir baada ya kusema kuwa suala hilo linapaswa lishughulikiwa na Tume ya Uchaguzi na Mipaka IEBC.

Kwa mujibu wa Chitembwe, mahakama hiyo ingelimulika suala hilo na kuingilia kati kwa kutumia sheria inayoipa mahakama uhuru wa kutathmini iwapo mwaniaji wa urais aneteuliwa na chama ametimiza vigezo vyote kikiwamo cha elimu.

Kuhusu suala la ufisadi, Jaji Chitembwe amekiri kwamba si rahisi kuukabili kikamilifu kwa wakati mmoja ila atahakikisha kwamba kesi zote zinazowasilishwa mbele yake zinatatuliwa kwa wakati ufaao. Amesema hilo litasaidia kuondoa dhana kwamba muda unaochukuliwa na mahakama kutoa uamuzi, ndio ambao umekuwa ukitumika kuwahonga majaji.

Chitembwe aidha ameongeza kwamba majaji wanapaswa kutoa sababu za msingi katika maamuzi wanayofanya ili kuhakikisha kwamba Wakenya wanapata majibu ya maswali yote wanayoibua baada ya maamuzi mbalimbali.

Wakati uo huo Chitembwe amekabiliwa na wakati mgumu kufafanua jinsi alivyoafikia uamuzi wa kuwataka wasanii kujichangulia mfumo wa kuwasilishwa kwa malipo yao pindi kazi zao zinapotumika na kampuni mbalimbali. Kesi hiyo inayohusu sheria za hakimiliki Copyright laws ilihusisha kampuni moja ya mwasiliano nchini mwaka 2016.

Aidha amekamilisha mahojiano yake kwa kuiambia Tume ya JSC kwamba hatafuti kazi katika Idara ya Mahakama kwa kuwa tayari anahudumu kama jaji na kwamba kilichomfanya kuwania wadhifa huo ni katika kuendeleza kazi nzuri inayotekelezwa na Idara ya Mahakama.

Share this: