×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

JSC kuanza mahojiano ya kujaza nafasi za Mahakama ya Juu

JSC kuanza mahojiano ya kujaza nafasi za Mahakama ya Juu

Tume ya Huduma za Mahakama JSC kuanza mahojiano ya kujaza nafasi ya aliyekuwa Jaji Jacktone Ojwang siku ya Jumatatu katika Mahakama ya Juu.

Jaji Ojwang' alistaafu mwezi  Februari mwaka wa 2020 baada ya kufikisha umri wa miaka sabini.

JSC imeratibu mahojiano hayo kufanyika kuanzia Jumatatu  hadi Jumatano ambapo watu wawili wawili watahojiwa kila siku.

Jumatatu itakuwa zamu ya Jaji Marete Njagi na Said Chitembwe ambao walijaribu kutafuta nafasi ya jaji mkuu bila kufaulu.

Jumanne, Jaji Nduma Nderi atahojiwa majira ya saa tatu asubuhi kabla ya Dkt. Nyaberi Patrick Lumumba kuhojiwa kuanzia saa tano.

Jumatano watakaohojiwa ni Jaji Ouko William Okello, Jaji Joseph Kiplagat na Bi Yano Alice Jepkoech ambao watafunga shughuli ya mahojiano hayo.

Watu tisa waliidhinishwa kuhojiwa japo ni saba pekee ambao watahojiwa kwa sababu tayari Jaji Martha Koome ameteuliwa na JSC kuchukua nafasi ya Jaji Mkuu hivyo kujaza nafasi iliyoachwa wazi na Davidi Maraga katika Mahakama ya Juu.

Hata hivyo, Jaji Kathurima Minoti alijiondoa licha ya awali jina lake kuidhinishwa.

Share this: