×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais Kenyatta apongezwa kwa kulegeza masharti ya Korona

Rais Kenyatta apongezwa kwa kulegeza masharti ya Korona

Muungano wa Mashirika ya Kijamii umekuwa wa hivi punde kupongeza hatua ya Rais Kenyatta kulegeza masharti ya kukabili maambukizi ya virusi vya Korona ili kuwapa nafasi Wakenya kujitafutia riziki.

Mwenyekiti wa Kitaifa wa Muungano huo Stephen Cheboi amesema kufungua kaunti tano zilizofungwa ambazo ni Nairobi, Kiambu, Kajiado, Machakos, na Nakuru, kutapunguza makali ya athari za Janga la Korona katika sekta mbalimbali za kibiashara.

Cheboi amesema kufungwa kwa kaunti hizo tano kuliathiri sekta mbalimbali, na kwamba Wakenya wanafaa kuzingatia masharti ya Wizara ya Afya ya kuzuia Korona ili kupunguza viwango vya maambukizi.

Haya yanajiri huku Wakenya wakiendelea kufurahia kutoka na hatua hiyo ambapo wahudumu wa bodaboda Mjini Thika, wamewasaidia maafisa wa polisi kuondoa vizuizi vya trafiki katika eneo la Chania, huku wakieleza jinsi walivyoathirika.

Share this: