×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Ruto abadili mbinu za kuingia Ikulu 2022

Ruto abadili mbinu za kuingia Ikulu 2022

Naibu wa Rais William Ruto amebadili mkondo wa kampeni na kuanza kuwasaka vigogo wa kisiasa katika maeneo mbalimbali nchini ili kufanikisha azimio lake la kuwania urais mwaka ujao.

Akizungumza baada ya kukutana na viongozi wa kaunti kumi na moja za eneo la Mlima Kenya, Ruto amekariri kwamba lengo lake kuu ni kuhakikisha anawaunganisha Wakenya wa matabaka mbalimbali.

Kwa mujibu wa Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichungwa, Ruto ametumia kikao hicho kufafanua mikakati ya jinsi ya kufufua uchumi ambao umeathiriwa na Janga la Korona, na hata kudokeza mbinu za kupunguza madeni ya serikali.

Aidha, viongozi wa Mlima Mkenya wa mrengo wa Tanga Tanga wamewasilisha matakwa yao kwa Ruto ambaye ameahidi kutimiza iwapo atafaulu kuwa rais ifikapo mwaka wa 2022.

Miongoni mwa matakwa hayo, ni kukiwamo kuwahusishwa wanasiasa wa eneo hilo katika kubuni serikali yake ili kukwamua uchumi ambao Mbunge wa Mathira Rigadhi Gachagua anasema umedorora wakati wa utawala wa Rais Uhuru Kenyatta.

Vilevile, Ruto amepanga kufanya mikitano katika maeneno ya Pwani, Magharibi na Nyanza ili kuwashawishi wanasiasa wengine kuunga maazimio yake.

Katika mkutano wa wiki iliyopita, wabunge sitini na wawili kutoka Mlima Kenya walifanya kikao katika boma la Gachagua, na kuafikiana kuhusu matakwa ambayo wangependa Ruto awatekeleezee baada ya kumuunga mkono.

Juma lililopita, Ruto aliteua kundi la wataalamu wa kiuchumi waliohudumu katika serikali ya Rais Mstaafu Mwai Kibaki ili kubuni sera za kukwamua uchumi endapo atakuwa rais.

Share this: