×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

DCI yaendeleza uchunguzi kufuatia mauaji ya Kitengela

DCI yaendeleza uchunguzi kufuatia mauaji ya Kitengela

Afisa mmoja wa polisi ambaye alihamishwa kutoka Nairobi, ni miongoni mwa watu wanaochunguzwa kufuatia kisa cha marafiki wanne kutoweka katika eneo la Kitengela kwenye kaunti ya Kajiado, kisha mili ya baadhi yao kupatikana maeneo tofauti wakiwa wameuliwa.

Inaarifiwa kwamba polisi huyo amekuwa akishirikiana na makundi ya majambazi ambao wamekuwa wakitekeleza uhalifu hapa Jijini Nairobi.

Afisa huyo alihamishwa baada ya kubainika kwamba amekuwa akitatiza juhudi za kuwanasa majambazi hao.

Aidha, imebainika kwamba wanne hao walikuwa wakihusishwa na tuhuma za uhalifu katika eneo la Pwani.

Miezi kadhaa iliyopita, wanne hao; Benjamin Imbayi, Elijah Obuong, Brian Oduor na Jack Ochieng, wamekuwa wakidaiwa kutekeleza uhalifu.

Aidha, imegundulika kwamba wanne hao ambao walitoweka baada ya kula chakula cha mchana tarahe 19 mwezi jana wakiwa Mjini Kitengela, wamekuwa wakipangia wizi katika Mtaa wa Donholm hapa Nairobi, kwa ushirikiano na polisi anayechunguzwa.

Imbayi ambaye alijulikana kwa jina Ramsey, anadaiwa kuwa miongoni mwa majambazi saba waliotekeleza wizi wa shilingi elfu mia tisa katika eneo la Ngong' kwenye kaunti ya Kajiado, mwezi Januari mwaka jana.

Aidha, ana kesi kadhaa za uhalifu katika Mahakama ya Kibra na Mavoko.

Mili mitatu iliyoaminika kuwa ya baadhi ya wanne hao ilipatikana katika maeneo ya Mathioya, kwenye kaunti ya Murang'a na Mjini Thika kwenye kaunti ya Kiambu, ambapo miwili imetambuliwa na familia kuwa ya Obuong' na Imbai.

Hata hivyo, mwili wa tatu uliofikirika kuwa wa Ochieng' umekataliwa na familia yake inayosema mwanao alikuwa na jeraha katika sehemu ya kifua na kwamba aliyepatikana hana alama hiyo.

Kwa sasa maafisa wa Idara ya Upelelezi DCI wanaendeleza uchunguzi ili kubaini kitendawili kinachozingira kutoweka kwa wanne hao.

Siku ya Ijumaa Inpekta Mkuu wa Polisi Hillary Mutyambai alimrisha DCI kutenga kikosi maalumu cha kukamilisha uchunguzi huo haraka iwezekanavyo.

Share this: