×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais wa Tanzania, Suluhu Hassan kufanya ziara ya kikazi Kenya

Rais wa Tanzania, Suluhu Hassan kufanya ziara ya kikazi Kenya

Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan atawasili nchini Jumanne wiki hii kwa ziara ya siku mbili.

Msemaji wa Ikulu Kanze Dena amesema Rais Suluhu atapokelewa na mwenyeji wake Rais Uhuru Kenyatta katika Ikulu ya Nairobi.

Ziara ya Suluhu inajiri kufuatia ujumbe wa Rais Kenyatta ulioongozwa na Waziri wa Michezo Amina Mohammed ambapo Kenyatta alimwalika Suluhu, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Kenyana Tanzania.

Wakati wa Ziara ya Waziri Mohammed, Suluhu aliiagiza Tume Maalum inayoshughulikia mahusiano baina ya mataifa haya mawili, kukutana na kupanga mikakati ya kuhakikisha uhusiano wa kidiplomasia unasalia imara.

Tume hiyo ambayo ilikutana mara ya  mwisho mwaka 2016 haijaweka wazi mikakati hiyo hadi sasa.

Mwezi uliopita Uganda na Tanzania zilitia saini mikataba mitatu yenye nia ya kuendeleza sekta ya mafuta na gesi. 

Mradi muhimu katika maelewano baina ya mataifa hayo ni ule wa ujenzi wa bomba la mafuta-ghafi lenye Kilometa 1, 443 kutoka Magharibi ya Uganda mpaka kwenye Bandari ya Bahari Hindi kule Tanga.

Ujenzi huo utagharimu dola za Marekani bilioni 3. 55, ambapo unatarajiwa kuwa mradi wenye bomba refu zaidi la mafuta duniani.

Ushirikiano huo wa kibiashara baina ya Tanzania na Uganda ulijiri baada ya jaribio la Kenya kutia saini mkataba kama huo na Uganda kugonga mwamba.

Suluhu ambaye ni Rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania aliapishwa Februari mwaka huu kufuatia kifo cha Hayati John Pombe Magufuli.

Share this: