×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

735 waambukizwa korona, 20 wafariki

735 waambukizwa korona, 20 wafariki

Wahudumu wa afya wameendelea kupongezwa kwa kujitolea katika vita dhidi ya korona.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, Waziri wa Afya Mutahi Kagwe amewataja wahudumu wa afya kuwa wafanyakazi waliohatarisha maisha yao tangu mwaka jana virusi hivyo viliporipotiwa nchini.

Kagwe aidha amewataka Wakenya kuendelea kuzingatia masharti ya kudhibiti maambukizi.

Haya yanajiri huku watu wengine mia saba na thelathini na watano wakiambukizwa virusi vya korona katika saa 24 zilizopita.

Idadi ya leo imetokana na vipimo vya sampuli elfu tano, mia saba hamsini na nane.

Viwango vya maambukizi leo ni asimilia 12. 8 ikilinganishwa na asilimia 9.7 ya jana.

Aidha, watu 224 wamepona ugonjwa wa Covid-19 na kufikisha idadi ya waliopona nchini kuwa elfu mia moja na nane, mia saba themanini na tisa.

Miongoni mwa waliopona leo hii, 177 walikuwa wakihudumiwa nyumbani, 47 wakiwa wale waliokuwa wamelazwa hospitalini.

Hata hivyo, wagonjwa ishirini wamefariki dunia kutokana na makali ya ugonjwa huo.

Idadi jumla ya walioaga dunia kutokana na COVID-19 nchini humu sasa ni elfu mbili, mia saba arubaini na wanne.

Wakati uo huo, wagonjwa mia moja themanini na wanane wako katika ICU. Thelathini na mmoja miongoni mwao wanatumia vipumuzi, mia moja kumi na watatu wanatumia oksijeni, arubaini na wanne wanahitaji uangalizi wa karibu.

Share this: