×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Kiunjuri aapa kupinga marekebisho ya katiba

Kiunjuri aapa kupinga marekebisho ya katiba

Kinara wa Chama cha The Service Party, TPS Mwangi Kiunjuri ameshikilia msimamo kwamba ataongoza kampeni za kupinga mchakato wa kuboresha katiba kupitia Mswada wa Marekebisho ya Katiba Mwaka wa 2020.

Akirejelea utata ambao umeibuka katika BBI ukiwamo mvutano kuhusu kubuniwa kwa mabunge mapya sabini, Kiunjuri amesema mivutano hiyo ni ishara tosha kwamba mswada huo haujazingatia maslahi ya wananchi.

Amesema eneo la Mlima Kenya litapinga BBI iwapo itaongozwa na matakwa ya wanasiasa wachache badala ya wananchi wanaolemewa na kodi.

Haya yanajiri huku Kiongozi wa Wachache katika Seneti James Orengo akidokeza kwamba Mswada wa BBI utapitishwa juma lijalo katika Bunge la Kitaifa sawa na Seneti.

Orengo ambaye amekuwa miongoni mwa washirika wa Kinara wa ODM Raila Odinga ambao wanashinikiza BBI kufanyiwa marekebisho, amesema mikakati imewekwa ili kuhakikisha mswada huo unapitishwa haraka iwezekanavyo.

Kwa upande wake Mbunge wa Rarieda Otiende Amollo amewashauri viongozi wenza katika eneo la Nyanza kuendelea kushirikiana ili kupitisha BBI pamoja na kuunga azimio la Raila kuwa rais mwaka ujao.

Aidha, Orengo ambaye pia ni Seneta wa Siaya amesema kura ya maamuzi itafanyika kati ya mwezi Julai na Agosti mwaka huu.

Katibu Mkuu wa COTU, Francis Atwoli amesema licha ya mivutano inayoshuhudiwa miongoni mwa wabunge, mswada huo utapitishwa.

Aidha, Atwoli amesema wengi wa Wakenya wanateseka kila baada ya uchaguzi mkuu hivyo sharti katiba ifanyiwe marekebisho ili kuhakikisha usawa, skisema COTU inaunga mkono BBI.

Ikumbukwe makundi yameendelea kujitokeza miongoni mwa wabunge na maseneta huku baadhi wakipinga pendekezo la BBI kurekebishwa na wengine wakishikilia kwamba lazima ipitishwe jinsi ilivyo.

Tayari seneti imeitisha kikao kingine maalum Alhamisi ijayo ili kuendelea kujadili BBI.

Share this: