×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Viongozi wa makanisa wamshukuru rais kwa kufungua maeneo ya kuabudu

Viongozi wa makanisa wamshukuru rais kwa kufungua maeneo ya kuabudu

Viongozi wa makanisa wamempongeza Rais Uhuru Kenyatta kufuatia agizo la kufunguliwa kwa maeneo ya kuabudu.

Wakiongozwa na Askofu Joel Kimani wa Kanisa la Huduma Revival Center mjini Ongata Rongai, katika Kaunti ya Kajiado, viongozi hao hata hivyo wamewataka wenzao kuhakikisha masharti ya kudhibiti maambukizi yanafuatwa.

Askofu Kimani amesisitiza umuhimu wa kuzingatia masharti hayo ili kupunguza viwango vya maambukizi.

Kauli sawa na hiyo imetolewa na Kasisi Grace Kimani ambaye amewashtumu Wakenya kwa kupuuza maagizo ya Wizara ya Afya.

Amewashauri kufanya kipaumbele afya yao, Kauli ambayo imewiana na ya Askofu Kinoti.

Vilevile tumezungumza na wamiliki wa baa na mikahawa mjini Ongata Rongai, ambao wameahidi kuzingatia masharti ya kudhibiti Korona.

Vilevile wametoa wito kwa wateja wao kufuata maagizo yote ili kuepuka maambukizi zaidi vilevile kusaidia sekta hiyo kuinuka kiuchumi.  

Share this: