×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais aongoza Maadhimisho ya Siku ya Leba katika Ikulu

Rais aongoza Maadhimisho ya Siku ya Leba katika Ikulu

Wakati uo huo, Rais Kenyatta ameongoza maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Leda Dei katika hafla ambayo imehudhuriwa na viongozi wachache kuambatana na masharti ya kudhibiti maambukizi ya Korona.

Hafla hiyo imefanyika katika Ikulu ya Nairobi, huku Rais Kenyatta akisema kwa mwaka wa pili Wafanyakazi wameathirika zaidi kutokana na Janga la Korona,  na kwamba wengi wamefutwa kazi huku uchumi ukidorora.

Rais amewapongeza wafanyakazi ambao wametumia nafasi zilizojitokeza wakati wa janga hili la korona kuwa wabunifu na kutafuta mbinu za kuleta suluhu.

Naibu wa Rais William Ruto hakuhudhuria hafla hiyo na badala yake kutumia mtandao wa Twitter kuwatakia wafanyakazi wote nchini heri za Leba Dei.

Katika ujumbe wake, Ruto amesema wafanyakazi wamechangia pakubwa katika maendeleo ya taifa licha ya changamoto ambazo zimesababishwa na Janga la korona.

Share this: