×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Maambukizi ya malaria yaongezeka huko Bungoma

Maambukizi ya malaria yaongezeka huko Bungoma

Maambukizi ya ugonjwa wa malaria yameripotiwa kuongezeka kwa asilimia kubwa katika Kaunti ya Bungoma hasa msimu huu wa mvua.

Kwa mujibu wa Msimamizi Mkuu wa Idara ya kukabili ugonjwa wa malaria katika Kaunti ya Bungoma Moses Wangusi, asilimia thelathini ya wagonjwa wanaofika katika Hospitali ya Rufaa ya Bungoma kila siku wanaugua ugonjwa huo.

Aidha, Wangusi anasema huenda idadi hiyo ikaongezeka vipindi vya mvua vinapoendelea kushuhudiwa.

Wakati ou huo, Wangusi amesema ni jukumu la kila mmoja kuzuia ugonjwa wa malaria kwa kuzingatia kanuni za Wizara ya Afya.

Share this: