×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Nani aliwaua wanaume wanne Kitengela

Nani aliwaua wanaume wanne Kitengela

Insepkta Mkuu wa Polisi, Hillary Mutyambai amemebuni kitengo maalumu cha polisi kuchunguza mauaji ya wanaume wanne baada ya kutoweka mjini Kitengela, Kaunti ya Kajiado.

Aidha, Mutyambai ameitaka Idara ya Upelelezi, DCI kushirikiana na kitengo hicho katika kubaini kiini cha mauaji hayo.

Akizungumza katika kituo cha mafunzo ya maafisa wa polisi cha Kiganjo kwenye Kaunti ya Nyeri, Mutyambai amesema polisi watahakikisha kuwa wanawakamata washukiwa waliotekeleza unyama huo.

Mili ya wanaume wawili ilipatikana katika hifadhi mbili za maiti kwenye Kaunti ya Murang'a na Kiambu.

Mwili wa Benjamini Imbayi mwenye umri wa miaka 30 ulipatikana katika msitu mmoja mjini Thika  huku wa mwenzake, Elijah Obuong mwenye umri wa miaka 35 ukipatikana karibu na mto.

Haya yanajiri huku familia ya mmoja wa wanaume waliotoweka; Jack Ochieng ikikana taarifa kwamba mwili uliopatikana katika hifadhi ya maiti huko Murang'a ni ya mpendwa wao.

Familia hiyo imesema mwili huo si wa Jack Ochieng na kuwapo polisi  kuwasaidia kumtafuta mpendwa wao. Donda Ochieng ni dadake Jack, Ochieng'

Wanne hao Benjamin Imbayi, Elijah Obuong, Brian Oduor na Jack Ochieng walianza kutafutwa baada ya jamaa zao kuripoti kwa polisi kuhusu kutoweka kwao.

Share this: