×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Hakuna mahusiano ya kimapenzi katika Idara ya Polisi-Matiang'i

Hakuna mahusiano ya kimapenzi katika Idara ya Polisi-Matiang'i

Huenda sheria za Idara ya Polisi zikafanyiwa marekebisho ili kuwazuia maafisa wa polisi kuwa na mahusiano ya kimapenzi.

Waziri wa Masuala ya Ndani ya Nchi Dakta Fred Matiang'i hatua hiyo itapunguza visa vya mauaji miongoni mwa maafisa hao ambavyo vimeendelea kukithiri.

Akizungumza alipofungua hafla ya mafunzo ya maafisa wa polisi kitengo cha Cadet katika chuo cha Mafunzo cha Kiganjo kwenye Kaunti ya Nyeri, Matiang'i aidha amesema kutazinduliwa kitengo kipya cha nidhamu kitakachoshughulikia visa vya dhuluma za kimapenzi hasa miongoni mwa maafisa wa polisi wa kike.

Kauli hii ya Matiang'i huenda ikaibua mjadala mkali humu nchini hasa ikizingatiwa imekuwa ikidaiwa polisi hutekeleza mauaji kutokana na mzongo wa mawazo. Wengi hulalamikia mazingira mabovu ya kufanyia kazi na hata mishahara  duni.

Visa  vya polisi kuwaua kwa kuwapiga risasi wapenzi wao, watoto na hata kujiua kutumia bunduki vimekuwa vikiongezeka nchini.

Cha hivi punde ni afisa wa polisi aliyekuwa mlinzi wa Matiangi aliyemuua mkewe, mwanao kabla ya kujiua.

Share this: