×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Wanasiasa waonywa dhidi ya kuingilia uongozi wa vyuo vikuu

Wanasiasa waonywa dhidi ya kuingilia uongozi wa vyuo vikuu

Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha amewaonya wanasiasa dhidi ya kuingilia uongozi wa vyuo vikuu nchini.

Akihutubu kwenye hafla ya kufuzu katika Chuo Kikuu cha Maseno, Waziri wa Elimu Profesa George Magoha amesema wanasiasa wameingiza ukabila vyuoni hali inayotishia kushuka kwa viwango vya elimu.

Kulingana naye, kila Mkenya ana haki ya kuhudumu katika eneo lolote hasa vyuoni iwapo amehitimu kimasomo na hana tajriba.

Aidha, ametoa tahadhari kwa maprofesa wanaozembea kazini kwamba watafutwa kazi.

Amesema kuwa viwango vya elimu vya maprofesa ambao hawajachapisha nakala zozote katika nyanja mbalimbali vinapaswa kutiliwa shaka.

Wakati uo huo, amewataka manaibu wakuu wa vyuo vikuu kukoma kuanzisha kozi nyingine bila ufahamu wa serikali. Pia ameonya kwamba wanaoanzisha mabewa kadhaa ya vyuo watakabiliwa kisheria kwani wanaiongezea serikali bajeti.

Share this: