×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

366 waambukizwa korona, 280 wapona, 18 wafariki

366 waambukizwa korona, 280 wapona, 18 wafariki

Watu mia tatu sitini na sita wameambukizwa virusi vya korona katika saa 24 zilizopita. Idadi ya leo imetokana na sampuli elfu tatu, mia sita sitini na nne zilizopimwa katika kipindi hicho.

Idadi ya maambukizi sasa ni elfu mia moja hamsini na moja, mia sita hamsini na tatu kote nchini. Viwango vya maambukizi navyo ni asilimia 10 kulinganishwa na asilimia 14.3 ya jana.

Katika taarifa, Wizara ya Afya vilevile imethibitisha kupona kwa watu mia mbili themanini na kufikisha jumla ya waliopona kuwa watu elfu mia moja na moja, mia sita arubaini na wawili kote nchini.

Miongoni mwa walioambukizwa leo hii, mia mbili na saba walikuwa wakihudumiwa nyumbani, 73 wakihudumiwa katika hospitali mbalimbali.

Kufikia sasa, watu elfu sabini na tatu, mia nane na watano wamehudumiwa na kupona nyumbani tangu kuripotiwa kwa korona nchini. Aidha, wengine elfu ishirini na saba, mia nane thelathini na saba wamepona hospitalini.

Pia kuna wagonjwa elfu moja, mia sita ishirini wamelazwa katika hospitali mbalimbali kutokana na ugonjwa wa covid-19. Elfu tano mia nane thelathini na wawili wanahudumiwa nyumbani.

Wakati uo huo, wagonjwa wengine mia mbili hamsini na wanne wako katika ICU, 56 miongoni mwao wanatumia vipumuzi, wengine 155 wanatumia oksijeni.

Wagonjwa wengine arubaini na watatu wanahitaji uangalizi wa karibu. Hata hivyo, wagonjwa kumi na wanane wamefariki kutokana na ugonjwa huo.

Kufikia sasa idadi ya vifo imefikia elfu mbili, mia nne themanini na kimoja.

Share this: