×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mtu mmoja afariki kufuatia ajali ya boti Lamu

Mtu mmoja afariki kufuatia ajali ya boti Lamu

Mwanamume mmoja amefariki dunia baada ya Boti kuzama kwenye eneo la Wiyoni katika Kaunti ya Lamu.

Mamlaka ya Ubaharia KMA imebainisha kwamba boti hilo ambalo lilikuwa likisafirisha viazi magunia 60 kutoka Mokowe kuelekea Lamu,  lilizidiwa na mawimbi makali ya bahari mwendo wa saa moja na nusu jana jioni kabla ya kuzama.

Mwili wa mwanamume huyo uliopolewa muda mfupi tu baada ya kuzama.

Watu wengine wawili waliokuwa ndani ya boti hilo wameokolewa ambapo hali zao zinaendelea kufuatiliwa katika Hospitali ya King Fahad.

KMA imesema mwili wa marehemu ambao umehifadhiwa katika Hospitali hiyo tayari umetambuliwa.

Kikosi cha Kitaifa cha Ulinzi wa Majini KCGS kinaendelea kuwatafuta jamaa wa marehemu ili kuwafahamisha kuhusu kifo cha mpendwa wao.

Share this: