×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Washiriki wa Odinga wazua migawanyiko kuhusu BBI, Kunani

Washiriki wa Odinga wazua migawanyiko kuhusu BBI, Kunani

Mswada wa Marekebisho ya Katiba mwaka wa 2020 kupitia mpango wa BBI unakumbwa na changamoto nyingine baada ya washirika wa Kinara wa ODM Raila Odinga kutofautiana vikali kuhusu iwapo mswada huo unaweza kubadilishwa au la.

Licha ya Mshauri wa kisheria wa Raila, Paul Mwangi kushikilia kwamba mapendekezo ya mswada huo hayafai kubadilishwa, hasa baada ya kuidhinishwa na zaidi ya mabunge ishirini na manne ya kaunti, mrengo wa Seneta wa Siaya James Orengo na Mbunge wa Rarieda Otiende Amolo unataka mswada huo urekebishwe kabla ya kura ya maamuzi.

Kwa mujibu wa Mwangi, kubadili baadhi ya mapendekezo huenda kukaathiri safari ya mapatano baina ya Rais Uhuru Kenyatta na Odinga tangu mwaka wa 2018, na kwamba itamaanisha mswada huo umetokana na maamuzi ya wachache bungeni badala ya maoni yaliyokusanywa nchini.

Mwangi anasema lazima wabunge wakubali kwamba ni wananchi ndio wenye mamlaka ya kuamua hatma ya BBI kupitia kura ya maamuzi wala si mashauriano ya wachache.

Hata hivyo, upande wa Orengo na Amolo nao unashinikiza BBI kufanyiwa marekebisho licha ya katiba kuwazuia wabunge kufanya hivyo, kwa misingi kwamba hatua hiyo itaipa bunge nguvu katika utungaji wa sheria kinyume na ilivyo sasa.

Aidha, Kiongozi wa Wachache katika Bunge la Kitaifa John Mbadiamedokeza kwamba kuna kikao maalumu cha kujadili ripoti ya Kamati ya Pamoja kuhusu BBI, huku Spika Justin Muturi akisema hana habari zozote kuhusu kikao hicho.

Imebainika kwamba kamati hiyo ya pamoja inayoshughulikia BBI, inalenga kukwepa kuwasilisha pendekezola kutaka BBI ifanyiwe marekebisho, ili usimamizi wa bunge la Kitaifa na Seneti uafikiane.

Ikumbukwe wabunge hawana mamlaka ya kubadili chochote katika BBI, hasa baada ya mabunge arubaini na matatu kuidhinisha mswada huo ambao umeaminika kuwa na maoni ya wananchi wa kawaida.

Share this: