×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Eliud Kipchoge ndiye mshindi wa Mbio za NN Marathon nchini Uholanzi

Eliud Kipchoge ndiye mshindi wa Mbio za NN Marathon nchini Uholanzi

Mshikilizi wa rekodi ya dunia katika mbio za marathon, Eliud Kipchoge ameibuka mshindi katika mbio za NN Marathon Mission leo hii.

Mbio hizo zimefanyika nchini Uholanzi.

Kipchoge ametumia muda wa saa mbili, dakika nne na sekunde thelathini pekee.

Kipchoge amezungumza muda mfupi uliopita huku akisema mbio hizo ni changamoto kuu katika maandaliza ya mbio za Tokyo.

Akihojiwa na wanahabari wa Shirika la BBC mapema jana, Kipchoge ambaye ni Mkenya amesema analenga kukimbia mbio hizo kwa ustadi mkubwa ili kuonesha dunia kwamba mwanadamu ana uwezo wa kukimbia mbio safi bila kutumia dawa zozote za kutitimua misuli.

Aidha, Kipchoge alielezea matumaini kwamba atashinda mbio hizo licha ya kwamba amekuwa akikumbukwa na changamoto hasa wakati huu dunia zima linapokabili janga la korona.

Mwaka uliopita, Kipchoge alishindwa kutetea ubingwa wake katika mbio za masafa marefu za London Marathon hivyo kuwavunja moyo mashabiki wengi duniani.

Kipchoge alishindwa na Raia wa Ethiopia Shura Kitata ambaye aliibuka mshindi kwa kuandikisha muda wa saa mbili  dakika tano na sekunde arubaini na moja. Mkenya Vincent Kipchumba alikuwa wa pili huku akiandikisha muda wa saa mbili dakika tano na sekunde arubaini na mbili.

Share this: