×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mwili wa Mwanamfalme Philip unazikwa Jumamosi

Mwili wa Mwanamfalme Philip unazikwa Jumamosi

Mwili wa mumewe Malkia wa Uingereza Elizabeth II, Mwanamfame Philip unazikwa leo hii.


Kulingana na ratiba iliyotolewa na Kasri ya Buckinham, ibada ya mazishi inatarajiwa kuanza saa tisa alasiri, sawa na saa kumi na moja jioni saa za Afrika Mashariki.

Hafla hii itahudhuriwa na watu thelathini pekee kuambatana na masharti ya kudhibiti maambukizi ya korona.

Ratiba hiyo inasema wanawe, ambao ni Mwanamfalme Charles, Andrew, Edward na Anne watalisindikiza jeneza  wakati wa hafla hiyo.

Wengine watakaokuwapo ni wajukuu wa Malkia ambao ni Wanamfalme William na Harry, watakaotembea kandokando ya gari aina ya Land Rover litakaloubeba mwili wa Mwanamfalme Philip kuelekea katika kanisa la St. upGeorge katika kasri ya Windsor. Malkia Elizabeth  ambaye ni mjane wa Philip ataketi kwenye hema peke yake.

Watu wengine wa karibu ndio watakaohudhuria hafla hiyo akiwamo mke wa Mwanamfalme Chalres, Camilla Duchess wa Cornwall, mume wa Bintimfalme Anne Timothy Laurence na mke wa Mwanamfalme Edward,  Sophie miongoni mwa wengine. Philip alifariki dunia wiki jana akiwa na umri wa miaka 99.

Share this: