×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×
Afisa wa KDF auliwa Baringo

Afisa Mmoja wa Jeshi la Ulinzi, KDF amefariki dunia kufuatia uvamizi wa wahalifu katika Kambi ya Jeshi ya Mukutani katika eneo la Baringo Kusini.

Chifu wa eneo la Mukutani, Benjamin Lecher, amesema wahalifu hao wanaodaiwa kutoka Jamii ya Pokot, walivamia kambi ya jeshi vilevile kukivamia Kituo cha Polisi wa Akiba NPR na wenzao wa RDU majira ya saa mbili usiku wa kuamkia leo.

Mapema leo, ufyatulianaji wa risasi baina ya maafisa wa polisi na wahalifu hao umeshuhudiwa huku mwili wa afisa aliyefariki dunia ukisalia katika eneo la tukio kwa muda.

Kulingana na ripoti ya Kituo cha Polisi cha Marigat, oparesheni ya kuwasaka wahalifu hao inaedelea.

Uvamizi huo unajiri siku chache tu baada ya Mshirikishi wa Utawala wa Eneo la Bonde la Ufa, George Natembeya kuagiza kurejelewa kwa oparesheni ya kuwakabili wahalifu wakiwamo wezi wa mifugo kufuatia utovu wa usalama.

Tangazo la Natembea lilijiri baada ya juhudi za viongozi wa eneo la hilo kushindwa kuafikiana jinsi ya kurejesha amani kwenye eneo hilo.


 

Share this: