×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sitafuti kazi, nataka kuhudumia umma -Philip Murgor

Sitafuti kazi, nataka kuhudumia umma -Philip Murgor

Wiki ya kwanza ya mahojiano ya wanaowania wadhifa wa Jaji Mkuu imekamilika huku Tume ya Huduma za Mahakama, JSC leo hii ikimhoji Wakili, Philip Murgor.

Murgor ambaye amewahi kuhudumu katika sekta ya umma kwa kipindi kirefu amekabiliwa na wakati mgumu kuyajibu maswali huku akikwepa kuyajibu baadhi.

Alipofika mbele ya JSC, Wakili Philip Murgor aliweka wazi kwamba lengo lake si kutafuta kazi bali kuihudumia umma.

Murgor aliyesisitiza kuwa amehitimu kuichukua nafasi hiyo, amelazimika kujitetea kuhusu matukio ya jaribio la kuipindua serikali mwaka 1982. Awali aliieleza JSC kwamba alikuwa miongoni mwa wanafunzi wa chuo kikuu waliokamatwa kwa kuhusishwa na jaribio hilo, ila wakaachiliwa miezi sita baadaye kutokana na ukosefu wa ushahidi.

Baadaye mwaka 1990 alipowa wakili wa serikali alikuwa kiongozi wa kesi kuhusu matukio hayo ambapo watu kadhaa walihukumiwa, ambao walidai kuteswa ili kukiri makosa. Jaji David Majanja alimtaka Murgor aeleze kwa kuzingatia matukio hayo iwapo anastahili kuwa Jaji kuu.

Murgor alijitetea akisema alikuwa tu akitekeleza majukumu yake.

Kabla ya hapo, wakili huyo alijipata pabaya alipokuwa akihojiwa na Kaimu Jaji Mkuu, Philomena Mwilu alipodai kuwa kuna pengo katika Idara ya Mahakama kwa kuwa hakuna Jaji Mkuu.

Ikumbukwe hapo Alhamisi JSC ilikataa ombi lililokuwa limewasilishwa na Murgor kumtaka Mwilu ajiondoe kwenye jopo linalofanya mahojiano hayo.

Si hayo tu alikwepa kuyajibu maswali kadhaa akidai majibu yake yanaweza kutumika baadaye kumkandamiza, mfano alipokuwa akijibu maswali ya Jaji Mohamed Warsame.

Kuhusu jinsi ambavyo ataimarisha utendakazi katika idara ya Mahakama akiwa Jaji Mkuu, ameahidi kushirikiana na idara nyingine, kukabili ufisadi, kushinikiza itengewe fedha za kutosha na kuhakikisha majaji arubaini na mmoja ambao hawajaapishwa hadi sasa, wanaapishwa.

Amejitetea dhidi ya maombi aliyowasilishwa mbele ya JSC na baadhi ya Wakenya waliotaka kuondolewa miongoni mwa watu walioidhinishwa kuhojiwa katika nafasi ya Jaji Mkuu.

Kando na Murgor waliohojiwa wiki hii ni Jaji Chitembwe Said Juma, Patricia Mbote, Jaji Martha Koome na Jaji Marete Njagi.

Wiki ijayo itakuwa zamu ya majaji Duma Nderi, William Ouko, Wakili Fred Ngatia, Profesa Moni Wekesa na Alice Yano. 

Wakili Philip Murgor ameapa kuwakabili mawakala anaodai wameiteka nyara Idara ya Mahakama iwapo ataidhinishwa kuwa Jaji Mkuu.

Akihojiwa wakati wa vikao vinavyoendelea kumtafuta atakaye mrithi David Maraga ambaye amestaafu mapema mwaka huu, Wakili Murgor amedai kwamba wapo mawakili wenye pesa ambao wamekuwa wakiingilia maamuzi muhimu mahakamani.

Amesema kuna uhuru katika Mahakama akisema ushirikiano baina ya Idara hiyo na nyingine haifai kufasiriwa kwamba kuna mwingiliano.

Kando na mahakama amesema atahakikisha kuna nidhamu miongoni mwa mawakili kwa kupendekeza sheria zinabuniwa kudhibiti miendendo yao ambayo inaweza kuathiri kazi za idara nzima.

Murgor amekuwa mtu wa tano kuhojiwa wiki hii baada ya Jaji Said Chitembwe, Patricia Mbote, Jaji Martha Koome na Jaji Marete Njagi.

 

Share this: