×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Rais Kenyatta atangaza nafasi wazi katika IEBC

Rais Kenyatta atangaza nafasi wazi katika IEBC

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa wazi nafasi 4 katika Tume ya Uchaguzi IEBC.

Katika Gazeti Ramsi la Serikali, Rais Kenyatta amewaalika watu kutuma maombi ili kufanyiwa mchujo wa kuwa makamishna wa IEBC.

Tangazo la Rais limejiri wakati ambapo IEBC imeanza mikakati ya kununua vifaa vya uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2022.

Ikumbukwe nafasi hizo zilisalia wazi baada ya makamishana Consolata Nkatha, Paul Kurgat na Margaret Mwachanya kujiondoa kwenye IEBC mnamo Aprili 16 2018 siku kadhaa tu baada ya Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati kutangaza kumwachisha kazi aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji, Ezra Chiloba.

Awali tarehe 18 mwezi Oktoba 2017,   Roselyn Akombe alitangaza kujiuzulu akiwa nje ya nchi kwa madai kwamba IEBC isingeaminika kiutendakazi baada ya kuuliwa kwa Chris Msando aliyekuwa Meneja wa Teknolojia na Mawasiliano. 

Makamikshna waliosalia ni Boya Molu na Abdi Guliye pamoja na Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati.

Share this: