×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

KCSE kuanza kusahishwa baada ya KCPE kutangazwa

KCSE kuanza kusahishwa baada ya KCPE kutangazwa

Waziri wa Elimu Prof. George Magoha amesema shughuli ya kusahisha karatasi za Mitihani ya KCSE itakamilika katika kipindi cha wiki tatu zijazo punde tu baada ya mitihani hiyo kukamilika.

Siku moja tu baada ya kutangaza matokeo ya Mtihani wa KCPE, Waziri Magoha amesifu jinsi mtihani wa KCSE ulivyofanywa licha ya baadhi ya maafisa wa serikali wakiwamo walimu kunaswa kutokana na madai ya wizi wa karatasi za mitihani.

Akizungumza Mjini Naivasha katika kaunti Nakuru baada ya kushuhudia ufunguzi wa karatasi za KCSE, Magoha amesema usalama umewekwa ili kuhakikisha usahishaji wa mitihani unaendelea jinsi ulivyopangwa.

Hata hivyo, Magoha ametoa onyo kali kwa walimu na maafsia wa serikali wanaopanga kushiriki katika wizi wa mitihani kwa kusambaza nakala kwenye mitandao ya kijamii.

Amesema uchunguzi unaendelea na kwamba watakaonaswa wataadhibiwa vikali kwa mujibu wa sheria.

Aidha, amesema walimu wote wataoshiriki katika shughuli hiyo watachanjwa dhidi ya COVID -19 na kuhakikisha masharti ya kukabili Korona yanazingatiwa kikamilifu.

Kuhusu usafiri wa wanafunzi hasa kutoka na kuingia kaunti tano zilizofungwa kufuatia masharti mapya ya Korona, Waziri Magoha amekariri kwamba serikali imeweka mikakati ya kuhakikisha watahiniwa wote wanarejea nyumbani kukiwamo kuwapa barua za kibali cha kusafiri.

Share this: