×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Sina mpango wa kuungana na Raila kwa sasa, Ruto asema

Sina mpango wa kuungana na Raila kwa sasa, Ruto asema

Naibu wa Rais William Ruto ameepuza madai kwamba amekuwa akifanya mashauriano na Kinara wa ODM Raila Odinga ili kubuni muungano wa kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2022.

Akirejelea mkutano wake wa hivi majuzi na Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya ambaye ni mshirika wa Odinga, Ruto amesema hajawahi kuzungumza na Oparanya kuhusu Odinga wala mipango ya kuungana na mrengo wa ODM..

Katika mahojiano na runinga moja nchini, Ruto amesema akimtazama Raila anamwona kuwa mshindani tu kisiasa wala si mshirika wa kuungana naye ifikapo 2022.

Kauli hii inajiri wakati kumekuwapo na mijadala mikali kuhusu ni nani atamuunga mwengine kuwa rais kati ya Ruto na Raila endapo wataaungana, ikizingatiwa kwamba Ruto haruhusiwi kisheria kuwa naibu wa rais kwa mara nyingine kikatiba, huku Raila ambaye ni mkongwe akifikirika kutaka urais pekee.

Vilevile, Ruto amekashifu usimamizi wa Chama cha Jubilee kwa misingi ya kuwanyanyasa baadhi ya wanachama kufuatia siasa za binafsi, na kudokeza kwamba iwapo Jubilee itasambaratika kabisa, basi atatumia chama cha UDA kuwania urais.

Aidha, amesema amekuwa akifanya mikutano ya faragha kutokana na visa ambapo washirika wake wamekuwa wakihangaisha na maafisa wa Idara ya Upelelezi DCI.

Licha ya uhusiano wake na Rais Uhuru Kenyatta kuendelea kutatizika na hata majukumu yake kupewa Waziri wa Usalama Dkt. Fred Matiang'i, Ruto ameshikilia kwamba bado Kenyatta ni rafiki na kuwa hapingi maamuzi yake licha ya kwenda kinyume na matarajio.

Amekariri kwamba Rais Kenyatta hana deni lake la kisiasa na kwamba ni Kenyatta mwenyewe alitoa ahadi ya kusema angemuunga kwa hiari baada ya kukamilisha miaka kumi ya uongozi.

Kuhusu chanjo ya COVID-19, Naibu wa Rais amesema hakualikwa kupata chanjo pamoja na watumishi wenza wa serikali ya kitaifa akiwamo Rais Kenyatta wiki tatu zilizopita.

Ametetea hatua yake ya kupata Chanjo ya Sputinik V badala ya Astrazeneca inayotolewa kwa wananchi, na kueleza haja ya serikali kuondoa masharti ya kuzuia uagizaji wa chanjo kwa wafanyabiashara binafsi.

Amesema siasa hazifai kuingizwa katika suala la chanjo

Share this: