×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mumo Faith Kawi mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kari Mwailu iliyoko kwenye Kaunti ya Makueni, ndiye mwanafunzi bora katika KCPE.

Mumo Faith Kawi mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kari Mwailu iliyoko kwenye Kaunti ya Makueni, ndiye mwanafunzi bora katika KCPE.

Mumo Faith Kawi mwanafunzi wa Shule ya Msingi ya Kari Mwailu iliyoko kwenye Kaunti ya Makueni, ndiye mwanafunzi bora katika Mtihani wa Kitaifa wa Darasa la Nane, KCPE baada ya kupata alama 433. Matokeo ya mtihani huo yaliyotangazwa na Waziri wa Elimu, Profesa George Magoha yanaonesha kwamba wasichana walitwaa nafasi nane bora miongoni mwa 15 bora huku wanafunzi katika shule za umma vilevile wakinakili matokeo bora katika orodha ya shule kumi na tano bora nchini. Rais Uhuru Kenyatta ameagiza watahiniwa wote wa KCPE wakabidhiwe matokeo licha ya wengine kuhusishwa katika udanganyifu.

Wasichana watatu wametwaa nafasi tatu za kwanza bora katika Mtihani wa KCPE wakiongozwa na Mumo Faith Kawi aliyepata alama 433.

Wesonga Yuvet wa Shule ya Msingi ya Chogoria aidha ni wa pili pamoja na  Murithi Angel wa Shule ya Wasichana ya Maseno, wote wakiwa na alama 432. Nafasi ya tatu ilimwendea Wanyonyi Mahanu Samuel akiwa na alama 431.

Aidha wavulana wamenakili matokeo bora katika mitihani ya hisabati, sayansi, mafunzo ya jamii na dini huku wasichana wakifanya vyema katika Kiingereza, Kiswahili na mitihani ya ishara. Vilevile matokeo masomo matano yameripotiwa kuimarika kulinganisha na mwaka 2019 huku matokeo duni vilevile yakiripotiwa kwenye masomo mengine matano.

Watahiniwa wenye mahitaji maalum vilevile wameng'aa kwenye mtihani huo.

Watahiniwa wote milioni moja, elfu mia moja sabini na tisa, mia moja tisini na wawili waliofanya Mtihani wa KCPE watajiunga na shule za upili, Waziri  Magoha akisema  hilo ni kutokana na mpango wa serikali wa kuhakikisha asilimia mia moja ya wanafunzi wa shule za msingi wanajiunga na shule za upili. Aidha Rais Uhuru Kenyatta ameagiza watahiniwa wote wakabidhiwe matokeo yao licha ya wengine kuhusishwa na visa vya udanganyifu.

Waziri ametangaza kwamba watahiniwa walifanya vyema katika mtihani huo licha ya janga la korona  na hapakuwa na tofauti kubwa na matokeo yaliyonakiliwa kwenye mitihani ya hapo awali. Amesema mitihani iliyofanywa  na watahiniwa baada ya kufunguliwa kwa shule kutokana na kufungwa kwa muda kutokana na korona, ilisaidia pakubwa kuwatayarisha kwa  KCPE.

Watahiniwa wameagiza kuchukua matokeo ya mitihani yao katika vituo walivyofanyia mitihani. Aidha ili kupata matokeo, tuma ujumbe mfupi wenye nambari ya usaji ya mtahiniwa ilifuatwa na jina KCPE kwa nambari 2006.

Share this: