×
x Digital News Videos Opinions Cartoons Education U-Report E-Paper Lifestyle & Entertainment Nairobian SDE Eve Woman Travelog TV Stations KTN Home KTN News BTV KTN Farmers TV Radio Stations Radio Maisha Spice FM Vybez Radio Enterprise VAS E-Learning Digger Classified The Standard Group Corporate Contact Us Rate Card Vacancies DCX O.M Portal Corporate Email RMS
Login ×

Mwanafunzi Lawrence Warunge akana mashtaka ya kuwaua jamaa zake

Mwanafunzi Lawrence Warunge akana mashtaka ya kuwaua jamaa zake

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu Lawrence Warunge, amekana mashtaka matano ya kuwaua jamaa zake wanne na mfanyakazi wa shambani mapema mwezi Januari mwaka huu. Warunge  mwenye umri wa miaka 22 amesomewa mashtaka dhidi yake baada ya ripoti ya uchunguzi wa kiakili aliofanyiwa katika Hospitali ya Mathari kuonesha kwamba hakuwa na matatizo ya kiakili.  

Awali alipofikishwa mahakamani mara ya kwanza baada ya kuwaua ndugu na wazazi wake kwa kuwadunga visu, hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo aliamuru afanyiwe uchunguzi wa kiakili kabla ya kutakiwa kukiri au kukana mashtaka dhidi yake. Ripoti ya kwanza ilionesha kwamba hangeweza kufunguliwa mashtaka na mahakama kuagiza atibiwe na kufuatiliwa kwa siku 30 kabla ya uchunguzi zaidi kufanywa.

Hapo jana faili iliyomzuia kufunguliwa mashtaka ilifungwa baada ya kubainika yuko na akili timamu. Ikumbukwe, alipokamatwa, Warunge alikiri kuhusika katika mauaji hayo na hata kuwaelekeza polisi alikozituma silaha alizotumia katika mauaji. Mpenziwe ambaye alishatiwa naye hapo awali, sasa atatumiwa kuwa shahidi wa upande wa serikali.

Kesi dhidi ya mshtakiwa itaendelea tarehe 11 mwezi Mei.  

Share this: